Imani ina thamani kubwa kuliko mali, wale wenye mali wana thamani machoni pa Mammon, wale wenye imani wana thamani machoni pa Yehova. - Enock Maregesi
Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. - Enock Maregesi
Watu wenye ujuzi au vipaji wanatakiwa kwenda shule kusomea ujuzi au vipaji vyao – kwa miezi mitatu au sita angalau. - Enock Maregesi
Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha. - Enock Maregesi