Quotation Explorer - 'Kwa'

Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake. - Enock Maregesi
Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC. - Enock Maregesi
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana. - Enock Maregesi
Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa. - Enock Maregesi
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi. - Enock Maregesi
Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. - Enock Maregesi
Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako. - Enock Maregesi
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu. - Enock Maregesi
Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia. - Enock Maregesi
Kuvunja sheria ni sawa na kufanya kosa, na kwa hiyo kuwa mkosaji, mbele ya sheria na mbele ya mungu. - Enock Maregesi
Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao. - Enock Maregesi
Ukitaka kumsahau mtu au kitu usimchukie au usikichukie kwa sababu kuchukia kuna nguvu sawa na kupenda. - Enock Maregesi
Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani. - Enock Maregesi
Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu. - Enock Maregesi
Kujiua ni ubinafsi kwa sababu ya watu wanaokupenda. - Enock Maregesi
Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii. - Enock Maregesi
Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano. - Enock Maregesi
Ukiwa mchapakazi hodari mwenye msimamo na nia thabiti ya utendaji kazi unaweza kuwa mpweke kwa maana ya kuwa na marafiki wachache. Lakini mashabiki utakuwa nao wengi. - Enock Maregesi
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake. - Enock Maregesi
Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauliwa na serikali zao. - Enock Maregesi
Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume. - Enock Maregesi
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya. - Enock Maregesi
Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha. - Enock Maregesi
Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke. - Enock Maregesi
Watu wenye ujuzi au vipaji wanatakiwa kwenda shule kusomea ujuzi au vipaji vyao kwa miezi mitatu au sita angalau. - Enock Maregesi
Wanaume wanaojiua kwa sababu ya mapenzi ni wanawake; wanawake wanaojiua kwa sababu ya fedha ni wanaume. - Panthera Tigrisi
Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini. - Enock Maregesi
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi. - Enock Maregesi
Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada. - Enock Maregesi
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi, si mimi. Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano, watakuwa na nguvu ya watu watano, watakuwa na nguvu ya ziada. - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi
Mawazo ya kukata tamaa yanaweza kusababisha tukamtengeneza au kumbuni tena Mungu kwa mfano wetu sisi wenyewe, mfano ambao kwa kawaida ni tofauti kabisa na mfano unaozungumzwa ndani ya Biblia. Hivyo tunaishia kutumikia mfano badala ya kumtumikia Mungu wa kweli. - Enock Maregesi
Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe. - Enock Maregesi
Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. - Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika kuingia na kutoka kwa hii pumzi. - Enock Maregesi
Fanya kazi kwa bidii leo, kuokoa kesho yako kesho. - Enock Maregesi
Ningependa maisha yangu yatakapokoma hapa duniani kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu. - Enock Maregesi
Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera. - Enock Maregesi
Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake. - Enock Maregesi
Wanaume hujiua kwa sababu ya fedha. Wanawake hujiua kwa sababu ya mapenzi. - Enock Maregesi
Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza. - Enock Maregesi
Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa. - Enock Maregesi
Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio. - Enock Maregesi
Fanya kazi kwa bidii na maarifa! - Enock Maregesi
Migogoro inatokea kwa sababu watu wameshindwa kuheshimiana. Ukijiheshimu na ukaheshimu wengine; utaacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta, wakati ukiingia. - Enock Maregesi
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu. - Enock Maregesi
Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu. - Enock Maregesi
Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake. - Enock Maregesi
Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. - Enock Maregesi
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu. - Enock Maregesi
Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi. - Enock Maregesi
Tukijifunza kuacha historia njema kwa kutenda mema katika maisha ya wengine itatuwezesha tuondoke duniani tukitabasamu na huku tukiwaacha wengi wakitokwa na machozi - Jacob Mushi
Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo. - Enock Maregesi
Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu. - Enock Maregesi
Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo. - Enock Maregesi
Tunapenda kuamini kwa sababu kuamini hurahisisha mambo… Usiamini. Jua. - Enock Maregesi
Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi. - Enock Maregesi
Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida. - Enock Maregesi
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake. - Enock Maregesi
Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue. - Enock Maregesi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru. - Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha. - Enock Maregesi
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa. - Enock Maregesi
Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo. - Enock Maregesi
Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. - Enock Maregesi
Kujitolea kwa moyo mmoja kwa muda mrefu huleta furaha na afya njema kwa mtoaji na kwa mpokeaji pia. - Enock Maregesi
Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia. - Enock Maregesi
Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. - Enock Maregesi
Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha. - Enock Maregesi
Click any word or name in a quote to explore, or search for more. [JSON] [SOURCE]