Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale. - Enock Maregesi
Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea. - Enock Maregesi
Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote. - Enock Maregesi