Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako! - Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha. - Enock Maregesi
Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi. - Enock Maregesi
Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake! - Enock Maregesi
Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake. - Enock Maregesi
Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha. - Enock Maregesi
Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi. - Enock Maregesi
Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia. - Enock Maregesi
Serikali imepewa mamlaka na wananchi kuwaendeshea nchi yao. Mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi. - Enock Maregesi
Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa. - Enock Maregesi
Kuleta mabadiliko katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuleta mabadiliko katika dunia leta mabadiliko katika nchi yako. - Enock Maregesi
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu. - Enock Maregesi