Utakapofika mwisho wa njia, geuka. Huo ndiyo mwanzo wa njia nyingine. - Enock Maregesi
Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya ufahamu wa mtu, binadamu angeshatengeneza ubongo. - Enock Maregesi
Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo. - Enock Maregesi
Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini. - Enock Maregesi
Mwisho wa sura si mwisho wa kitabu. Fungua ukurasa mwingine. - Enock Maregesi
Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha. - Enock Maregesi
Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi. - Enock Maregesi
Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu. - Enock Maregesi
Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu. - Enock Maregesi
Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Allaah Tabaraka wa Ta`Ala {The Absolute Divine UnNamed} DOES NOT test to "See" if you're worthy of Jannaah or Jahannam ! If only one can perceive this, one knows it is one that places oneself in either station !! - AainaA-Ridtz
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya. - Enock Maregesi
Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. - Enock Maregesi
Hekima ni ufunguo wa kufanya maamuzi mema kulingana na msingi wa maarifa ya Biblia. - Enock Maregesi
Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida. - Enock Maregesi
Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi. - Enock Maregesi
Kabbalah' ni sayansi ya Mti wa Uzima wa Milele wa Bustani ya Edeni au 'The Tree of Life of the Garden of Eden' katika mbingu ya nne, ambayo ni ramani ya ulimwengu na roho ya mwanadamu; au Sayansi ya Mungu, uchawi wa kujua 99% ya siri ya uumbaji wa Mungu. - Enock Maregesi
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana. - Enock Maregesi
Nje ya uwezo wa kisheria ni shetani. - Enock Maregesi
Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke. - Enock Maregesi
Uko wapi ubinadamu wa watu? - Enock Maregesi
Ukisema ukweli utapata uhuru wa nafsi. Ukisema uongo utapata uhuru wa umma. Heri uhuru wa nafsi kuliko wa umma. - Enock Maregesi
Kanuni za fasihi ndiyo msingi wa maandiko yote ya kitaalamu hapa ulimwenguni. Watu hawana budi kuzifuata kanuni hizo kama wanataka kutumia vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa. - Enock Maregesi
Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo. - Enock Maregesi
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake. - Enock Maregesi
Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda. - Enock Maregesi
Ukiwapa watoto wako uhuru wa shaghalabaghala au uhuru wa kila kitu watajisahau! Wape uhuru wa mahesabu. - Enock Maregesi
Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao. - Enock Maregesi
Heri kuwa Mkristo wa Yesu Kristo, au Mwislamu wa Mtume Muhammad, kuliko kuwa mkristo wa kanisa au mwislamu wa msikiti. - Enock Maregesi
Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia. - Enock Maregesi
Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu. - Enock Maregesi
Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa. - Enock Maregesi
Kuwa mkristo wa kanisa au wa dini ni kughushi imani – na kughushi imani ni dhambi kubwa. - Enock Maregesi
Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani! - Enock Maregesi
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu. - Enock Maregesi
Mawazo ya kukata tamaa yanaweza kusababisha tukamtengeneza au kumbuni tena Mungu kwa mfano wetu sisi wenyewe, mfano ambao kwa kawaida ni tofauti kabisa na mfano unaozungumzwa ndani ya Biblia. Hivyo tunaishia kutumikia mfano badala ya kumtumikia Mungu wa kweli. - Enock Maregesi
Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. - Enock Maregesi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru. - Enock Maregesi
Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha. - Enock Maregesi
Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Nina matatizo ya kiafya: Udadisi wa hali ya juu wa kiakili. - Enock Maregesi
Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauliwa na serikali zao. - Enock Maregesi
Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii. - Enock Maregesi
Kushukuru wakati wa matatizo ni kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi. - Enock Maregesi
Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Mwachie mwanao urithi wa kutosha ili aweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili asiweze kufanya kitu. - Enock Maregesi
Mtu yoyote anayedanganya ni Shetani, kwani Shetani ni baba wa uongo. Tusikubali kudanganywa ovyo, hasa watoto wetu, katika kipindi hiki cha utandawazi na teknolojia. - Enock Maregesi
Marafiki zako wa mwanzo ni wazuri kuliko wote. - Enock Maregesi
Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa. - Enock Maregesi
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako. - Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera. - Enock Maregesi
Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu – Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani. - Enock Maregesi
Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu. - Enock Maregesi
Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta. - Enock Maregesi
Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera. - Enock Maregesi
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka. - Enock Maregesi
Mungu ni mwandishi wa hadithi ya maisha yangu na ndiye anayeandika ukurasa wa mwisho. - Enock Maregesi
Kafara ya maombi ni kushukuru wakati wa matatizo. Kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba. - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi
Dunia – Mfumo wa Jua wa Sol – Solar Interstellar Neighborhood – Njiamaziwa – Local Galactic Group – Virgo Supecluster – Local Supercluster – Ulimwengu unaoonekana – Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu. - Enock Maregesi
Sentensi ni mkusanyiko wa maneno unaoanza na herufi kubwa na kuisha na alama ya kushangaa, kuuliza, au nukta. Sentensi bora ni fupi, angavu, sahihi, yenye mantiki, na kamilifu. - Enock Maregesi
Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza. - Enock Maregesi
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu. - Enock Maregesi
Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake. - Enock Maregesi
Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa. - Enock Maregesi
Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda. - Enock Maregesi
Kitabu cha 'Kolonia Santita' ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania. - Enock Maregesi
Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu chochote. Wanaweza kuona tusipoweza kuona – nyuma na mbele ya tarehe zetu za kuzaliwa. - Enock Maregesi
Wape watoto uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa shaghalabaghala. - Enock Maregesi
Watu hawashabikii watu wa kawaida; wanashabikia watu ambao si wa kawaida. - Enock Maregesi
Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, binadamu angeshatengeneza moyo. - Enock Maregesi
Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio. - Enock Maregesi