Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini. - Enock Maregesi
Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada. - Enock Maregesi
Lengo la jina la kitabu ni kuishawishi hadhira kusoma dibaji, na lengo la dibaji ni kuishawishi hadhira kusoma salio la kitabu kizima. - Enock Maregesi
Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu. - Enock Maregesi
Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu. - Enock Maregesi
Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue. - Enock Maregesi