Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo. - Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha – na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Kafara ya maombi ni kushukuru wakati wa matatizo. Kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba. - Enock Maregesi
Ukitaka kumsahau mtu au kitu usimchukie au usikichukie kwa sababu kuchukia kuna nguvu sawa na kupenda. - Enock Maregesi
Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa. - Enock Maregesi
Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza – zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Kuna watu wanatumia nguvu nyingi nyingi kusafisha kilichopita na kusahau kama hakuna marudio,usikumbuke ya yaliyopita bali jifunze kupita hayo. - Chrisper Malamsha
Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi. - Enock Maregesi
Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada. - Enock Maregesi
Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana. - Enock Maregesi
Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba. - Enock Maregesi
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi, si mimi. Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano, watakuwa na nguvu ya watu watano, watakuwa na nguvu ya ziada. - Enock Maregesi
Tumaini lina nguvu kuliko woga… Usisimame. Endelea kutembea. - Enock Maregesi
Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano. - Enock Maregesi