Quotation Explorer - 'Maisha'

Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka. - Enock Maregesi
Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni. - Enock Maregesi
Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia. - Enock Maregesi
Tukijifunza kuacha historia njema kwa kutenda mema katika maisha ya wengine itatuwezesha tuondoke duniani tukitabasamu na huku tukiwaacha wengi wakitokwa na machozi - Jacob Mushi
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu. - Enock Maregesi
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake. - Enock Maregesi
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi. - Enock Maregesi
Watu wanapokuwa katika migogoro maisha yao hutakiwa kurahisishwa. Kuna ukingo mwembamba kati ya uzima na wazimu. - Enock Maregesi
Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea. - Enock Maregesi
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu. - Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha. - Enock Maregesi
Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda. - Enock Maregesi
Mimi ni mmoja kati ya wale wasiopenda maendeleo ya watu wachache au peke yako ndomana nimechagua mabadiliko katika maisha yangu sisubirii wanasiasa - Chrisper Malamsha
Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako. - Enock Maregesi
Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka. - Enock Maregesi
Ukiwa na mawazo hasi utakuwa na maisha hasi, na ukiwa na mawazo chanya utakuwa na maisha chanya. - Enock Maregesi
Usiifundishe familia yako anasa. Ifundishe upendo, unyenyekevu na hofu ya Mungu. Ukiifundisha anasa utahatarisha maisha ya mbinguni ya familia yako, na ya kwako pia. - Enock Maregesi
Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako kuelekea kwenye takdiri yako utaishi kama Shetani anavyotaka, si kama Mungu anavyotaka. - Enock Maregesi
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako. - Enock Maregesi
Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani. Ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso. - Enock Maregesi
Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli? - Enock Maregesi
Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa. - Enock Maregesi
Mungu ndiye aliyetengeneza ubongo. Ni vizuri kuamini kwamba Yeye ndiye anayetupa maarifa, kupitia malaika wema, kuhusu maisha yetu na kuhusu siri ya uumbaji wake. - Enock Maregesi
Kuikaribisha amani ya Mungu katika maisha yangu kumenisaidia. Naishi mbinguni duniani. - Enock Maregesi
Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi. - Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa. - Enock Maregesi
Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda. - Enock Maregesi
Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha. - Enock Maregesi
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika kuingia na kutoka kwa hii pumzi. - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi
Ningependa maisha yangu yatakapokoma hapa duniani kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu. - Enock Maregesi
Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii. - Enock Maregesi
Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu. - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha. - Enock Maregesi
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa. - Enock Maregesi
Mungu ni mwandishi wa hadithi ya maisha yangu na ndiye anayeandika ukurasa wa mwisho. - Enock Maregesi
Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale. - Enock Maregesi
Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. - Enock Maregesi
Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa. - Enock Maregesi
Click any word or name in a quote to explore, or search for more. [JSON] [SOURCE]