Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. - Enock Maregesi
Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. - Enock Maregesi
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya. - Enock Maregesi
Maskini hajali wewe ni nani. Anajali utu ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. - Enock Maregesi
Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera. - Enock Maregesi
Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri. - Enock Maregesi
Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. - Enock Maregesi
Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. - Enock Maregesi
Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. - Enock Maregesi
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka. - Enock Maregesi
Kila kipato kina mashetani yake, mengine mazuri na mengine mabaya, lakini mengi ni mabaya. Wakati mwingine maskini ahitaji pesa, pesa anaweza kushindwa kuidhibiti, anahitaji paa na kuta nne kujisetiri yeye na familia yake. - Enock Maregesi
Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. - Enock Maregesi