Ukila kiapo fanya kile ulichoahidi katika kiapo, si kinyume chake hata kidogo, hata kama dunia haitakubaliana na wewe. - Enock Maregesi
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana. - Enock Maregesi
Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui! - Enock Maregesi
Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo. - Enock Maregesi
Maskini hajali wewe ni nani. Anajali utu ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli? - Enock Maregesi
Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu. - Enock Maregesi
Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida. - Enock Maregesi
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake. - Enock Maregesi