Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu. - Enock Maregesi
Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda. - Enock Maregesi
Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe. - Enock Maregesi
Maendeleo ya mtu yatatokana na juhudi za mtu mwenyewe. - Enock Maregesi
Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui! - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi