Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu. - Enock Maregesi
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika – kuingia na kutoka kwa hii pumzi. - Enock Maregesi
Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo. - Enock Maregesi
Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii. - Enock Maregesi
Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui! - Enock Maregesi