Quotation Explorer - 'Yako'

Mimi ni mmoja kati ya wale wasiopenda maendeleo ya watu wachache au peke yako ndomana nimechagua mabadiliko katika maisha yangu sisubirii wanasiasa - Chrisper Malamsha
Geuza hasira yako kuwa hekima. - Enock Maregesi
Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe. - Enock Maregesi
Kuleta mabadiliko katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuleta mabadiliko katika dunia leta mabadiliko katika nchi yako. - Enock Maregesi
Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa. - Enock Maregesi
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika kuingia na kutoka kwa hii pumzi. - Enock Maregesi
Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia. - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako kuelekea kwenye takdiri yako utaishi kama Shetani anavyotaka, si kama Mungu anavyotaka. - Enock Maregesi
Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale. - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi
Usiifundishe familia yako anasa. Ifundishe upendo, unyenyekevu na hofu ya Mungu. Ukiifundisha anasa utahatarisha maisha ya mbinguni ya familia yako, na ya kwako pia. - Enock Maregesi
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake. - Enock Maregesi
Ndoto yako haitakufa mpaka utakapokufa. Usikate tamaa, kabisa! - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha. - Enock Maregesi
Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani. - Enock Maregesi
Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake! - Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa. - Enock Maregesi
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana. - Enock Maregesi
Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka. - Enock Maregesi
Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko Injili. Mungu hasisimuliwi na matatizo yako. Anasisimuliwa na imani yako. - Enock Maregesi
Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida. - Enock Maregesi
Akili yako isipokuwa timamu, familia itakushinda. Familia ikikushinda utalaumiwa na Mwenyezi Mungu. - Enock Maregesi
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako. - Enock Maregesi
Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako! - Enock Maregesi
Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii. - Enock Maregesi
Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako. - Enock Maregesi
Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako. - Enock Maregesi
Fanya kazi kwa bidii leo, kuokoa kesho yako kesho. - Enock Maregesi
Click any word or name in a quote to explore, or search for more. [JSON] [SOURCE]