Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni. - Enock Maregesi
Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha. - Enock Maregesi
Mtu yoyote anayedanganya ni Shetani, kwani Shetani ni baba wa uongo. Tusikubali kudanganywa ovyo, hasa watoto wetu, katika kipindi hiki cha utandawazi na teknolojia. - Enock Maregesi
Biblia ni kiwanda cha imani. - Enock Maregesi
Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma. - Enock Maregesi
Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale. - Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo! - Enock Maregesi
Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine kulinda thamani ya utu wako. - Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera. - Enock Maregesi
Kitabu cha 'Kolonia Santita' ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania. - Enock Maregesi
Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani! - Enock Maregesi
Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha. - Enock Maregesi
Udadisi ni kiboko cha ujinga. - Enock Maregesi
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi. - Enock Maregesi
Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa. - Enock Maregesi
Ukienda katika kituo cha watoto yatima halafu watoto wakakulilia shida zao na ukaondoka bila kuwasaidia chochote, hutalala vizuri usiku. - Enock Maregesi