Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue. - Enock Maregesi
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, masaa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safiri salama. - Enock Maregesi
Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani! - Enock Maregesi