Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka. - Enock Maregesi
Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu. - Enock Maregesi
Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta. - Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha. - Enock Maregesi
Mawazo ya kukata tamaa yanaweza kusababisha tukamtengeneza au kumbuni tena Mungu kwa mfano wetu sisi wenyewe, mfano ambao kwa kawaida ni tofauti kabisa na mfano unaozungumzwa ndani ya Biblia. Hivyo tunaishia kutumikia mfano badala ya kumtumikia Mungu wa kweli. - Enock Maregesi
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake. - Enock Maregesi