Quotation Explorer - 'Enock Maregesi'

Heri kuwa Mkristo wa Yesu Kristo, au Mwislamu wa Mtume Muhammad, kuliko kuwa mkristo wa kanisa au mwislamu wa msikiti. - Enock Maregesi
People think that other international languages are smarter and more business wise. But they have to understand that we have to preserve our culture. - Enock Maregesi
Kama umefanya au umesema kitu kibaya na ukasema ukweli mbele ya mtu au ya watu, omba msamaha kupata tena kibali cha umma. - Enock Maregesi
Kabbalah' ni sayansi ya Mti wa Uzima wa Milele wa Bustani ya Edeni au 'The Tree of Life of the Garden of Eden' katika mbingu ya nne, ambayo ni ramani ya ulimwengu na roho ya mwanadamu; au Sayansi ya Mungu, uchawi wa kujua 99% ya siri ya uumbaji wa Mungu. - Enock Maregesi
Usuluhishi ni dawa ya uhusiano mwema miongoni mwa watu. - Enock Maregesi
Ukiwanyima watoto uhuru wa kuwa watoto leo watakuwa na uhuru wa kuwa watoto kesho. - Enock Maregesi
Ukikosana na mwanamke usimpige mchana. Mpige usiku. Ukimpiga mchana watu watasema umemwonea. Ukimpiga usiku watu watasema huenda alikuwa na makosa. Wanawake hawatakiwi kupigwa. - Enock Maregesi
Mtu akikutukana mwambie asante au samahani. Asante au samahani vina nguvu kuliko kuomba (asikutukane) au kutukana. - Enock Maregesi
Katika umoja hakuna 'umimi', kuna 'sisi kwa pamoja'; na lengo la umoja ni kutengeneza nguvu, ya ziada. - Enock Maregesi
Tunasema uongo kwa sababu hatuna ujasiri wa kusema ukweli. Ukweli hautupi uhuru, unatupa upweke. - Enock Maregesi
Mtu akikushauri kufanya kitu ambacho ni kinyume na takdiri ('destiny') ya maisha yako, hata kama huyo mtu hana nia mbaya na wewe, sema 'hapana' kwa hiyo 'ndiyo' yake. - Enock Maregesi
Maskini hutamani mambo mazuri ya wakati uliyopita. Tajiri hutamani mambo mazuri ya wakati unaokuja. - Enock Maregesi
Falsafa ya Usawa kwa Watu na Vitu Vyote ya Yin-Yang ya Kichina ni falsafa inayotumiwa na Wachina, kujifunza sanaa ya mapigano na kutengeneza madawa ya asili, na magaidi wa madawa ya kulevya wa Amerika ya Kusini na Kaskazini kusaidia watu waliosahauliwa na serikali zao. - Enock Maregesi
Hadithi ya maisha yangu ni yangu. Wewe ni nani kusema hadithi yangu si ya kweli? - Enock Maregesi
Kila kipato kina mashetani yake, mengine mazuri na mengine mabaya, lakini mengi ni mabaya. Wakati mwingine maskini ahitaji pesa, pesa anaweza kushindwa kuidhibiti, anahitaji paa na kuta nne kujisetiri yeye na familia yake. - Enock Maregesi
Natafuta mwanamke mwenye utu, wema, uaminifu na tabia njema sifa ambazo ataendelea kuwa nazo hata uzeeni. Sifa hizi zinaweza kubadilika kwa sababu ya maisha au kwa sababu ya mapenzi ya Mungu, lakini mabadiliko haya hayatakuwepo kwa haraka. Sura haidumu. Tabia hudumu. - Enock Maregesi
Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi. - Enock Maregesi
Kigumu kuliko vyote ni kizuri kuliko vyote. - Enock Maregesi
Watu wakikuonyesha tabia zao za ndani kabisa waamini. Wanajijua vizuri zaidi, kuliko unavyowajua. - Enock Maregesi
Usifanye kazi peke yako wala usiwe mbinafsi! Washirikishe wenzako kukamilisha malengo madhukura ya kadari ya maisha yako. - Enock Maregesi
Usitukane kamwe. Pigana itakapobidi. - Enock Maregesi
Kutunza siri wakati mwingine ni kitu kigumu sana kwa baadhi ya watu lakini watu wanapaswa kuwa na uwezo wa kutunza siri kujijengea uaminifu, ambao ni siri ya mafanikio. - Enock Maregesi
Mungu ni mwingi wa hekima, lakini kwa nini alimuumba Shetani? Kwa sababu, Shetani wakati mwingine ni hekima. Ukiendelea kupigwa, bila wewe kupiga, unaweza kuumia, familia yako inaweza kuumia pia! Kuepusha matatizo ya familia yako, wakati mwingine unahitaji kupigana. - Enock Maregesi
Tambua vitu vya muhimu katika maisha yako ijapokuwa unaweza kuacha alama katika dunia bila kujitambua baada ya kuondoka. - Enock Maregesi
Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko Injili. Mungu hasisimuliwi na matatizo yako. Anasisimuliwa na imani yako. - Enock Maregesi
Wananchi wakiamua kufanya kitu katika nchi yao kwa asilimia 100 serikali, na taasisi zake zote, haitaweza kuwazuia. Kwa sababu, mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Kushirikiana na maadui wa nchi yetu ni hatia ya kosa la uhaini. Adhabu yake ni kifo, au kifungo cha maisha. - Enock Maregesi
Ukiwa mchapakazi hodari mwenye msimamo na nia thabiti ya utendaji kazi unaweza kuwa mpweke kwa maana ya kuwa na marafiki wachache. Lakini mashabiki utakuwa nao wengi. - Enock Maregesi
Watu hawashabikii watu wa kawaida; wanashabikia watu ambao si wa kawaida. - Enock Maregesi
Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya mtu baada ya mtu kufariki? Kwa nini watu wana kawaida ya kuona thamani ya pumzi katika kipindi ambacho mtu hana uwezo tena wa kuvuta hewa? Nini thamani ya pumzi? Thamani ya pumzi ni kukufanya uwe wewe na si udongo. - Enock Maregesi
Kuzaliwa na kuishi ni mibaraka mikubwa ya Mwenyezi Mungu kuliko yote duniani. - Enock Maregesi
Dunia imekata tamaa. Matatizo ya watu yamekuwa makubwa kuliko ukombozi wa maisha yao. Sekunde moja ya toba inaweza kukupa ufalme wa mbinguni. Hujachelewa. - Enock Maregesi
Mungu alitengeneza familia. Alitengeneza koo, makabila na mataifa, ili watu wajuane na kuheshimiana. - Enock Maregesi
Ukitaka kujua maana halisi ya maisha yako kuwa tayari kufanya vitu vikubwa vitakavyohitaji nguvu ya Mungu kuvikamilisha na kudumu katika maisha hayo kwa kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Kafara ya maombi ni kushukuru wakati wa matatizo. Kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba. - Enock Maregesi
Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine. - Enock Maregesi
Ndoto yako haitakufa mpaka utakapokufa. Usikate tamaa, kabisa! - Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo! - Enock Maregesi
Watu wanapokuwa katika migogoro maisha yao hutakiwa kurahisishwa. Kuna ukingo mwembamba kati ya uzima na wazimu. - Enock Maregesi
Kolonia Santita ina sura 8 na kila sura ina faslu 3. - Enock Maregesi
Dunia Mfumo wa Jua wa Sol Solar Interstellar Neighborhood Njiamaziwa Local Galactic Group Virgo Supecluster Local Supercluster Ulimwengu unaoonekana Ulimwengu. Huu ndiyo ukoo wa dunia yetu. Chochote alichokifanya Yoshua kilitokea katika ukoo huu. - Enock Maregesi
Ser bom para o ambiente. Seja gentil com os animais. Seja gentil com as pessoas. Se você fizer isso, você vai deixar uma marca no mundo. - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako maisha yako yatakubadilisha. - Enock Maregesi
Nimewapa watoto wangu kila kitu katika maisha isipokuwa umaskini. Lakini bado wamenishinda. - Enock Maregesi
Wape watoto wako urithi wa kutosha ili waweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili wasiweze kufanya kitu. Wape watoto uhuru wanaostahili kupata, uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa kila kitu. - Enock Maregesi
Watu wenye ujuzi au vipaji wanatakiwa kwenda shule kusomea ujuzi au vipaji vyao kwa miezi mitatu au sita angalau. - Enock Maregesi
Dikteta ni kiongozi anayetawala nchi kwa amri yake peke yake bila ya kushauriwa na mtu, hasa yule aliyeingia madarakani kwa mtutu wa bunduki. Dikteta uchwara si dikteta, ni dikteta nusu. - Enock Maregesi
Siku ya kuzaliwa ni siku ya kwanza ya safari nyingine ya siku 365, masaa 5, dakika 48, sekunde 46 na maili milioni 600 kulizunguka jua. Safiri salama. - Enock Maregesi
Mtu akikutukana mwambie asante. Akikupiga mwambie asante. Akiendelea kukupiga, pigana. - Enock Maregesi
Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume. - Enock Maregesi
Maskini hajali wewe ni nani. Anajali utu ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Sentensi ni mkusanyiko wa maneno unaoanza na herufi kubwa na kuisha na alama ya kushangaa, kuuliza, au nukta. Sentensi bora ni fupi, angavu, sahihi, yenye mantiki, na kamilifu. - Enock Maregesi
Usiwapoteze marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wako, wala usiwaache marafiki zako wa mwanzo kwa sababu ya ujinga wao. - Enock Maregesi
Uko wapi ubinadamu wa watu? - Enock Maregesi
Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Fanya kazi kwa bidii leo, kuokoa kesho yako kesho. - Enock Maregesi
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. 2 + 2 = 5. Umoja una sisi, si mimi. Watu wanne wakifanya kazi kwa ushirikiano, watakuwa na nguvu ya watu watano, watakuwa na nguvu ya ziada. - Enock Maregesi
Kujiua ni ubinafsi kwa sababu ya watu wanaokupenda. - Enock Maregesi
Tumaini lina nguvu kuliko woga… Usisimame. Endelea kutembea. - Enock Maregesi
Maskini hudhani tajiri ana tabia ya kuringa. Tajiri hupenda kuzungukwa na watu sahihi wenye mawazo sawa na ya kwake. - Enock Maregesi
Ukienda katika kituo cha watoto yatima halafu watoto wakakulilia shida zao na ukaondoka bila kuwasaidia chochote, hutalala vizuri usiku. - Enock Maregesi
Kusaliti nchi, ambayo majeshi ya ulinzi na usalama yameundwa kuilinda, ni miongoni mwa makosa makubwa kabisa kuweza kufanywa na mtu! Adhabu yake ni kifungo cha maisha jela, au kunyongwa hadi kufa. - Enock Maregesi
Mawazo ya kukata tamaa yanaweza kusababisha tukamtengeneza au kumbuni tena Mungu kwa mfano wetu sisi wenyewe, mfano ambao kwa kawaida ni tofauti kabisa na mfano unaozungumzwa ndani ya Biblia. Hivyo tunaishia kutumikia mfano badala ya kumtumikia Mungu wa kweli. - Enock Maregesi
Ijapokuwa maombi ya sifa yana nguvu kuliko maombi ya kushukuru, kushukuru kuna nguvu kuliko kuomba. - Enock Maregesi
Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa. - Enock Maregesi
Kitabu cha 'Kolonia Santita' ni kitabu cha wasomi na wasiokuwa wasomi, watu wa mijini na watu wa vijijini, watu wazima, vijana na watoto. Hadhira ya kitabu hiki ni jamii nzima ya Tanzania. - Enock Maregesi
Kujamiiana si anasa tena katika maisha yangu. Ni hitaji muhimu kwa ujenzi wa familia. - Enock Maregesi
Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine kulinda thamani ya utu wako. - Enock Maregesi
Kuleta mabadiliko katika dunia si lazima upate nafasi katika dunia. Kuleta mabadiliko katika dunia leta mabadiliko katika nchi yako. - Enock Maregesi
Kitu kikishindikana katika maisha yako kamwe usikate tamaa kwa sababu kushindwa ni mama wa mafanikio na kukata tamaa ni mama wa kushindwa. - Enock Maregesi
Ukitaka kumjua mwanamke jua historia yake. - Enock Maregesi
Wengine hatuishi kama wafalme kwa sababu ya nguvu za giza zilizopo kati ya Mungu na wanadamu. Nyota zetu zimefunikwa. Una kila kitu unachotafuta, ndani ya moyo wako. Usitafute furaha, utajiri au amani nje ya moyo wako. Tafuta furaha, utajiri au amani ndani ya moyo wako. - Enock Maregesi
Kwa nini tuseme a.k.a na si k.k.k au k.n.k au k.a.k? Lazima tujifunze kuipenda na kuitetea lugha yetu kwa usumbufu wa vizazi vijavyo. - Enock Maregesi
Kuzaliwa ni heshima kubwa tulivyopewa sisi wanadamu. Tafuta nafasi katika nchi yako, kuacha alama katika dunia. - Enock Maregesi
Maskini huamini unahitaji pesa kupata pesa. Tajiri huamini utapata pesa kwa kutumia pesa za wengine. - Enock Maregesi
Sikujui. - Enock Maregesi
Jambazi aliyekubuhu hawezi kumuua mtu bila kumwambia kwa nini anamuua. Si sheria ya John Murphy. Ni sheria ya EAC. - Enock Maregesi
Tunazaliwa na kufa. Lakini hatujui tunakotoka. Wala hatujui tunakokwenda. Huenda tunatoka na kwenda katika dunia nyingine, ya ulimwengu mwingine, hivyo kutufanya wageni wa dunia yetu wenyewe. Acha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta. - Enock Maregesi
Acha alama katika dunia baada ya kuondoka. - Enock Maregesi
Kuwa mkristo wa kanisa au wa dini ni kughushi imani na kughushi imani ni dhambi kubwa. - Enock Maregesi
Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu. - Enock Maregesi
Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa. - Enock Maregesi
Ukiwa na mawazo hasi utakuwa na maisha hasi, na ukiwa na mawazo chanya utakuwa na maisha chanya. - Enock Maregesi
Kuandika hadithi ni kitu kimoja. Kuweka kanuni za fasihi katika hadithi ni kitu kingine. - Enock Maregesi
Kuvunja sheria ni sawa na kufanya kosa, na kwa hiyo kuwa mkosaji, mbele ya sheria na mbele ya mungu. - Enock Maregesi
Sikujui. Lakini naamini hungependa kuishi maisha yako hapa duniani bila kuacha urithi au kumbukumbu ya aina yoyote katika jamii. - Enock Maregesi
Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya moyo wa mtu, binadamu angeshatengeneza moyo. - Enock Maregesi
Usiangalie nyuma kujutia vitu ulivyovifanya, angalia nyuma kujifunza kutokana na makosa uliyofanya. - Enock Maregesi
Heri kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka, kuliko kusema mbele za watu kwamba pesa haijakupa furaha. Wengi hupata jeuri ya kusema hivyo kutokana na umaskini wa watu wanaowazunguka. - Enock Maregesi
Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu. - Enock Maregesi
Lengo la jina la kitabu ni kuishawishi hadhira kusoma dibaji, na lengo la dibaji ni kuishawishi hadhira kusoma salio la kitabu kizima. - Enock Maregesi
Mwaka mmoja na nusu unatosha kumjua mwanamke kabla ya ndoa. Miezi sita itakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mchumba. Mwaka mmoja na nusu utakufanya ujue kama mwanamke anaweza kuwa mke. - Enock Maregesi
Kama huwezi kumpenda mtu usimchukie. - Enock Maregesi
Hufanani na yoyote katika dunia hii. Unafanana na wewe mwenyewe. Usimdharau mtu, humjui! - Enock Maregesi
Wanaume hujiua kwa sababu ya fedha. Wanawake hujiua kwa sababu ya mapenzi. - Enock Maregesi
Ndani ya sekunde moja baada ya ulimwengu wetu kuumbwa, miaka bilioni kumi na tatu nukta saba tano iliyopita, chembe zote ndogo zinazopatikana ndani ya atomu zilitengenezwa. Zote hizo zimeshapatikana isipokuwa 'Higgs Boson', na 'Higgs Boson' ndiyo ya muhimu kuliko zote. - Enock Maregesi
Wanaume hupenda nyama kwenye mifupa. - Enock Maregesi
Shetani angekuwa na uwezo wa kuona ndani ya ufahamu wa mtu, binadamu angeshatengeneza ubongo. - Enock Maregesi
Serikali imepewa mamlaka na wananchi kuwaendeshea nchi yao. Mamlaka ya wananchi hushinda ya serikali. - Enock Maregesi
Waandishi ni wadadisi. - Enock Maregesi
Ningependa maisha yangu yatakapokoma hapa duniani kukumbukwa kama mtu aliyejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake wote, kutumia kipaji alichopewa na Mungu. - Enock Maregesi
Usipobadilisha maisha yako kuelekea kwenye takdiri yako utaishi kama Shetani anavyotaka, si kama Mungu anavyotaka. - Enock Maregesi
Shetani hana uwezo wa kupandikiza chuki au upendo au kitu chochote ndani ya moyo wa mtu, bila mtu mwenyewe kupenda. - Enock Maregesi
Maendeleo ya mtu yatatokana na juhudi za mtu mwenyewe. - Enock Maregesi
Kwa sababu ya udadisi wa hali ya juu nasoma kila kitu ninachokutana nacho hasa vile visivyonipendeza. Ukitaka kupata maarifa usisome tu vitabu vinavyokupendeza. Soma vitabu visivyokupendeza. - Enock Maregesi
Wakati mwingine tukitaka kutambulika hatuna budi kuweka mbele aibu ya heshima yetu. - Enock Maregesi
Watu wanahitaji elimu na ajira kuwaepusha na janga la madawa ya kulevya. - Enock Maregesi
Shetani ni mungu wa dunia hii kwa wale wasiomwamini Mungu. Kwa wale wanaomwamini Mungu, Mungu ndiye Mungu wa dunia hii. - Enock Maregesi
Kwa mwanamke wa kuoa natafuta hasanati. Akiwa mbaya atakuwa mzuri. Akiwa maskini atakuwa tajiri. Akiwa gumbaru atakuwa msomi. Akiwa mshamba atakuwa mjanja. Akiwa mjinga atapata maarifa. Nitampenda zaidi kwa mazuri kuliko mabaya. - Enock Maregesi
Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni kifo. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni uzima wa milele. Kikwazo kikubwa cha kwenda mbinguni ni Shetani. Kikwazo kikubwa cha kwenda ahera ni Yesu Kristo. Yesu Kristo ni njia iliyo huru ya kwenda mbinguni. Shetani ni njia iliyo huru ya kwenda ahera. - Enock Maregesi
Kanuni za fasihi ndiyo msingi wa maandiko yote ya kitaalamu hapa ulimwenguni. Watu hawana budi kuzifuata kanuni hizo kama wanataka kutumia vipaji vyao katika ngazi ya kimataifa. - Enock Maregesi
Mtu yoyote anayedanganya ni Shetani, kwani Shetani ni baba wa uongo. Tusikubali kudanganywa ovyo, hasa watoto wetu, katika kipindi hiki cha utandawazi na teknolojia. - Enock Maregesi
Mdanganyifu hudanganya wanaopenda kudanganywa. - Enock Maregesi
Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu. - Enock Maregesi
Maisha ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni. - Enock Maregesi
I wanted to do something new. The world is becoming a global village and we have to understand these different cultures. There is a Danish culture, an Israeli culture and so on. So if you want to go to Denmark, then read the book. - Enock Maregesi
Marafiki zako wa mwanzo ni wazuri kuliko wote. - Enock Maregesi
Ukiwapa watoto wako uhuru wa shaghalabaghala au uhuru wa kila kitu watajisahau! Wape uhuru wa mahesabu. - Enock Maregesi
Nilijitolea sehemu ya maisha yangu ya kijamii na kifamilia kuweza kuchapisha Kolonia Santita katika kiwango nilichokitaka. - Enock Maregesi
Ukisema ukweli utapata uhuru wa nafsi. Ukisema uongo utapata uhuru wa umma. Heri uhuru wa nafsi kuliko wa umma. - Enock Maregesi
Mungu alikupa vipaji ili uwanufaishe wengine na si kujinufaisha mwenyewe, na aliwapa wengine vipaji ili kukunufaisha wewe na si kujinufaisha wenyewe, kwa lengo la kuleta mabadiliko chanya katika dunia yetu. - Enock Maregesi
Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake. - Enock Maregesi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa baba kwa familia yake. Kwa Tanzania alikuwa mlezi; wa ndoto ya haki, amani, uzalendo, ujamaa, na uhuru. - Enock Maregesi
Msamaha si kwa ajili ya watu wenye mabawa ya kuku, ni kwa ajili ya watu wenye macho ya tai. Kua kuujua msamaha. - Enock Maregesi
Mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia. - Enock Maregesi
Mtu aliyepoteza kazi na mke na watoto wake kuuwawa kwa mfano, watu wanapaswa kuwa makini na yeye, ana uwezo wa kufanya chochote. - Enock Maregesi
Ukiwapa watu kile wanachokitaka wataendelea kukihitaji. - Enock Maregesi
Usiifundishe familia yako anasa. Ifundishe upendo, unyenyekevu na hofu ya Mungu. Ukiifundisha anasa utahatarisha maisha ya mbinguni ya familia yako, na ya kwako pia. - Enock Maregesi
Ukitaka kumsahau mtu au kitu usimchukie au usikichukie kwa sababu kuchukia kuna nguvu sawa na kupenda. - Enock Maregesi
Kushukuru wakati wa matatizo ni kafara ya maombi. - Enock Maregesi
Fanya kazi kwa bidii na maarifa! - Enock Maregesi
Dunia ni uwanja wa vita wa vita ya dhambi ya vita ya maisha! Kuishi maisha ya kufikirika ni kushinda vita ya maisha ya vita ya dhambi. Vita ya dhambi ya vita ya maisha si vita ya kufikirika! Bila Yesu katika maisha yetu hakuna atakayeishinda. - Enock Maregesi
Maskini hutengeneza pesa kwa kufanya kazi asizozipenda. Tajiri hutengeneza pesa kwa kufanya kazi anazozipenda. - Enock Maregesi
Akili yako isipokuwa timamu, familia itakushinda. Familia ikikushinda utalaumiwa na Mwenyezi Mungu. - Enock Maregesi
Maombi yako yasipojibiwa usikate tamaa, Mungu alishakusikia na tayari alishaandaa malaika wa kukuletea jibu. Jibu wakati mwingine huchelewa kufika kwa sababu ya nguvu za giza. Usiwe na haraka, muda wako ukifika utajibiwa. - Enock Maregesi
Hekima ni ufunguo wa kufanya maamuzi mema kulingana na msingi wa maarifa ya Biblia. - Enock Maregesi
Baada ya Adam na Hawa kutenda dhambi katika bustani ya Edeni, kila mtu anayezaliwa anazaliwa katika dhambi. Kwa hiyo dhambi hutokana na maisha, na maisha hutokana na dhambi. - Enock Maregesi
Maskini mwenye pesa nyingi ni tajiri bahili. Tajiri mwenye mifuko iliyotoboka ni tajiri badhiri. - Enock Maregesi
Kujitolea kwa moyo mmoja kwa muda mrefu huleta furaha na afya njema kwa mtoaji na kwa mpokeaji pia. - Enock Maregesi
Hatutakiwi kuishi kama raia wa Tanzania peke yake. Tunatakiwa kuishi kama raia wa dunia na watumishi wa utu, hasa katika kipindi hiki cha zama za utandawazi. Sina lazima ya kutoka nje kufanya utafiti wa kazi zangu siku hizi. Nje ninayo hapa ndani! - Enock Maregesi
Ukila kiapo fanya kile ulichoahidi katika kiapo, si kinyume chake hata kidogo, hata kama dunia haitakubaliana na wewe. - Enock Maregesi
Mheshimu sana mtu aliyekupandisha juu kwa sababu utakaposhuka ndiye atakayekupokea, ijapokuwa unaweza usishuke kabisa au unaweza kushuka ukapokelewa na mtu mwingine baki, kwa kudura za Mwenyezi Mungu. - Enock Maregesi
Kuwa makini na kila kitu unachofanya kwa maana ubongo ni kitu cha ajabu, ubongo una uwezo wa kukupotosha. - Enock Maregesi
Maisha ni kani au 'force' ya kipekee zaidi katika ulimwengu unaofahamika; achilia mbali changamani ('complexity') na kutapakaa ('diversity') zaidi kuliko kani zote! Ni tukio la ajabu kuliko matukio yote yaliyowahi kutokea. - Enock Maregesi
Ujasusi ni kitu cha muhimu kwa maendeleo ya nchi yoyote. Watu wanaoshughulika na ujasusi wanapaswa kuwa makini mno kwani kazi yao ni nyeti sana kulinganisha na kazi za watu wengine. Kosa dogo la kiusalama linaweza kubadili mwelekeo wa historia ya nchi. - Enock Maregesi
Katika maisha watu watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi. - Enock Maregesi
Nje ya uwezo wa kisheria ni shetani. - Enock Maregesi
Mimi ni mwana wa Mungu. Sisi sote ni watoto wa Mungu. Lengo la kuzaliwa kwangu ni kufanya kazi pamoja na Roho Mtakatifu na malaika kumtumikia Bwana, na kueneza injili ya Yesu Kristo duniani kote, kupitia vitabu. - Enock Maregesi
Heri kuwa maskini kwa miaka mingi duniani na kuwa tajiri wa milele mbinguni kuliko kuwa tajiri kwa miaka mingi duniani na kuwa maskini wa milele ahera. - Enock Maregesi
Nina matatizo ya kiafya: Udadisi wa hali ya juu wa kiakili. - Enock Maregesi
Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale. - Enock Maregesi
Soma vitabu visivyopendeza vilivyoandikwa na waandishi mahiri. - Enock Maregesi
Serikali mara nyingi hutegemea ujasusi wa ndani na nje kufanya maamuzi mazito na sahihi ya kuendesha nchi. - Enock Maregesi
Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu chochote. Wanaweza kuona tusipoweza kuona nyuma na mbele ya tarehe zetu za kuzaliwa. - Enock Maregesi
Imani huchukua miaka mingi kuijenga lakini sekunde chache kuibomoa. - Enock Maregesi
Maamuzi ya Adamu na Hawa ya kutokumtii Mungu juu ya Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya, ndiyo yaliyosababisha Yesu Kristo ajitolee maisha yake ili wengine waweze kuishi. Hakuna Mungu bila Yesu. Mtafute Yesu, kukomboa sura na asili ya Mungu. - Enock Maregesi
Imani ni nia ya kujua kisichoweza kujulikana na hupeleka watu kwenye ukweli. Kuamini hupotosha, na ni nia ya kudharau kinachoweza kujulikana. - Enock Maregesi
Ukiipenda sana nchi yako ni rahisi sana kuichukia serikali yake! - Enock Maregesi
Shindana na wenzako kuwa juu zaidi katika tasnia uliyojichagulia. - Enock Maregesi
Ukifanya maamuzi kubaliana na matatizo yake. - Enock Maregesi
Kuikaribisha amani ya Mungu katika maisha yangu kumenisaidia. Naishi mbinguni duniani. - Enock Maregesi
Ukitaka kutambulika usione aibu. - Enock Maregesi
Mtu anayesema pesa haijampa furaha hana nia ya kusaidia watu. - Enock Maregesi
Kula sana ni kujichimbia kaburi kwa meno yako mwenyewe. - Enock Maregesi
Pesa ina maana kwa sababu ya wanawake. - Enock Maregesi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa bendera ya taifa letu! Alikuwa alama ya amani, haki, uhuru, ujamaa, uzalendo, na Tanzania. - Enock Maregesi
Maskini hufanya kazi kwa bidii kupata pesa. Tajiri hutumia pesa kupata pesa. - Enock Maregesi
Afrika isomeshe watu wake, na itumie vizuri mapato yanayotokana na mauzo ya rasilimali zake kwa faida ya jumla ya wananchi wa nchi zake, kusudi baadaye wawe wataalamu wa rasilimali za nchi zao wenyewe, kuepukana na utumwa wa rasilimali. Rasilimali za Afrika zina miiko na masharti yake. - Enock Maregesi
Mwanamke akikuomba pesa, mpe! - Enock Maregesi
Mwachie mwanao urithi wa kutosha ili aweze kufanya kitu, lakini si urithi wa kutosha ili asiweze kufanya kitu. - Enock Maregesi
Ni rahisi kushinda vita ya maisha na kuishi mbinguni duniani. Ni vigumu kushinda vita ya dhambi na kuishi mbinguni paradiso. - Enock Maregesi
Ndoto ni lugha ya roho inayozungumza kimafumbo kumfanya binadamu ajitambue. - Enock Maregesi
Maskini hufundisha watoto wake jinsi ya kupambana na maisha. Tajiri hufundisha watoto wake jinsi ya kuwa matajiri. - Enock Maregesi
Mungu alisema tupendane katika shida na raha; Luka 6:27-36. Katika matatizo mpende hasimuyo. Maumivu ya watu hufanana. - Enock Maregesi
Uwezekano wa watoto wa ukoo mmoja kuoana ni mkubwa kwa sababu damu ina nguvu ya uvutano. Kuhakikisha kwamba familia zinafahamiana na kushirikiana katika mambo mbalimbali ni jukumu la wazazi. - Enock Maregesi
Your dreams won’t die until you die don’t ever stop believing! - Enock Maregesi
Tumaini ni injini ya imani. - Enock Maregesi
Wananchi wataendelea kuwepo hata kama serikali haitakuwepo. Serikali haiwezi kuwashinda wananchi. Sauti ya umma ni sauti ya Mungu. Serikali haiwezi kumshinda Mungu. - Enock Maregesi
Udadisi ni kiboko cha ujinga. - Enock Maregesi
Biblia ni kiwanda cha imani. - Enock Maregesi
Waandishi wanapaswa kuwa wadadisi, kama paka, ijapokuwa udadisi ni hatari. - Enock Maregesi
Wape watoto uhuru wa mahesabu, lakini si uhuru wa shaghalabaghala. - Enock Maregesi
Maskini ana mawazo ya kupata pesa bila kufanya kazi. Tajiri ana mawazo ya kupata pesa kwa kufanya kazi. - Enock Maregesi
Mungu ndiye aliyetengeneza ubongo. Ni vizuri kuamini kwamba Yeye ndiye anayetupa maarifa, kupitia malaika wema, kuhusu maisha yetu na kuhusu siri ya uumbaji wake. - Enock Maregesi
Kujenga urafiki na wanasiasa wakati mwingine ni kitu kizuri. Wanasaidia kurahisisha mambo. - Enock Maregesi
Novelists and the literary world play an important part in shaping languages. The Swahili they write influence the readers and their languages. The literary obstacle in Tanzania is not that people do not read, but that they don’t read because there are no interesting writers. - Enock Maregesi
Mwisho wa sura si mwisho wa kitabu. Fungua ukurasa mwingine. - Enock Maregesi
Geuza hasira yako kuwa hekima. - Enock Maregesi
Serikali inayodhulumu wananchi wake ni hatari kuliko simba. - Enock Maregesi
Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu. - Enock Maregesi
Unaweza kusaliti nchi kwa sababu za kiitikadi, kisiasa, matatizo ya akili, au pesa. Ukifanya hivyo na ukabainika; utawajibika kwa adhabu ya kifo, au maisha. - Enock Maregesi
Migogoro inatokea kwa sababu watu wameshindwa kuheshimiana. Ukijiheshimu na ukaheshimu wengine; utaacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta, wakati ukiingia. - Enock Maregesi
Utakapofika mwisho wa njia, geuka. Huo ndiyo mwanzo wa njia nyingine. - Enock Maregesi
Kati ya nchi yako na serikali yako ni kitu gani unakipenda zaidi? Ipende zaidi nchi yako, kuliko serikali yako! - Enock Maregesi
Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kupata sifa ya madaraka na hivyo kunyanyasa na kudharau watu kwa sababu ya madaraka yake, bali alichaguliwa kuleta mabadiliko katika dunia kama Rais wa Tume ya Dunia kutetea afya na amani ya dunia nzima kwa unyenyekevu na heshima kwa binadamu wenzake. - Enock Maregesi
Be nice to the environment. Be nice to animals. Be nice to people. If you do that, you will leave a mark on the world. - Enock Maregesi
Ukiwa na kipaji nenda shule kurekebisha kipaji chako, ukiwa na ujuzi nenda shule kurekebisha ujuzi wako. - Enock Maregesi
Mungu ni mwandishi wa hadithi ya maisha yangu na ndiye anayeandika ukurasa wa mwisho. - Enock Maregesi
Mungu akikuweka mahali unapostahili kuwa, kulingana na takdiri ya maisha yako, hakuna mtu mwenye uwezo wa kushindana na kipaji chako. - Enock Maregesi
Silaha kuu ya uchoyo ni kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Ni upendo. - Enock Maregesi
Halafa hailipi. - Enock Maregesi
Njia rahisi ya kujua maana ya ndoto zako ni kurekodi ndoto zako kila siku asubuhi, au kila unapoota, kwa angalau majuma mawili. Baada ya muda huo ndoto zako zitaanza kuleta maana. Lengo lake kubwa ni kukufanya ujitambue. - Enock Maregesi
Tunapenda kuamini kwa sababu kuamini hurahisisha mambo… Usiamini. Jua. - Enock Maregesi
Maumivu ya matatizo ya yule aliyekukosea hayana tofauti na maumivu ya matatizo ya wewe uliyekosewa. Adui yako (kwa mfano) akifiwa na mke aliyempenda sana, atajisikia vibaya kama utakavyojisikia vibaya kufiwa na mke uliyempenda sana. Kuwa na huruma kwa waliokukosea, wakati wa shida. - Enock Maregesi
Tumia pesa kibahili, si kibadhiri. - Enock Maregesi
Mbili jumulisha mbili wakati mwingine si sawa na nne. Ni sawa na nne jumulisha moja kwa sababu moja ni nguvu ya ushirikiano. - Enock Maregesi
Hutaweza kufikia malengo yako kikamilifu bila msaada wa wataalamu Hata kama una kipaji au ujuzi kiasi gani. - Enock Maregesi
Imani ina thamani kubwa kuliko mali, wale wenye mali wana thamani machoni pa Mammon, wale wenye imani wana thamani machoni pa Yehova. - Enock Maregesi
Watu hubariki wenzao ambao ni wakarimu, na hulaani wenzao ambao ni wabahili. Ukiwa mkarimu kwa watu umekopa neema kutoka kwa Mungu, na Mungu atakulipa kutokana na matendo yako. - Enock Maregesi
Ikiwa hakuna kitu kinafanyika katika maisha yako usijali. Kuna kitu kinafanyika kuingia na kutoka kwa hii pumzi. - Enock Maregesi
Toa msamaha kwa waliokukosea kwa sababu dhambi zilizofanya mkosane zilitoka kwa Shetani. - Enock Maregesi
Dictatorial government is more dangerous than lions! - Enock Maregesi
Tumia kipaji ulichopewa na Mungu. - Enock Maregesi
Kuna mafanikio ya aina mbili hapa duniani: Mafanikio ya Shetani na mafanikio ya Mungu. Mafanikio ya Shetani ni rahisi kupata na ni ya kitumwa. Mafanikio ya Mungu ni magumu kupata lakini ni ya hakika. Mungu akikubariki, pesa inaongezeka kama inavyoongezeka saa. - Enock Maregesi
Lengo la kuabudu ni kumtukuza, kumheshimu, kumsifia, kumfurahia, na kumpendeza Mungu. Ibada yetu lazima ionyeshe mapenzi ya kweli na uaminifu mkubwa kwa Mungu kwa ajili ya wema na rehema ambavyo ametupa kupitia Mwanaye wa Pekee aliyekufa msalabani, ili kutuokoa kutoka ubinafsini. - Enock Maregesi
Hakuna maana yoyote kupambana na Shetani katika dunia hii ambapo yeye ndiye mtawala. Pambana na Shetani katika dunia ya kiroho ambapo Shetani hana nguvu yoyote dhidi ya Yesu Kristo. - Enock Maregesi
Nitajisikia raha sana kufungwa kwa ajili ya matatizo watu. - Enock Maregesi
Toa msaada katika jamii iliyosaidia kukulea ulipokuwa mdogo. - Enock Maregesi
Click any word or name in a quote to explore, or search for more. [JSON] [SOURCE]